Viongozi kukutana kujadili shughuli za AMISOM nchini Somalia.

1 Agosti 2013

Marais sita kutoka  mataiafa yanayochangia wanajeshi nchini Somalia chini ya kikosi cha AMISOM  wanakutana mjini Kampala Uganda mwishoni mwa wiki hii kwa kikao cha dharura kuzungumzia  jitihada zonazoendelea za kukabilina na kundi la wanamgambo wa al Shabaab.Mkutano huo ambao utaongozwa na rais wa Uganda Yoweri Museveni unajiri baada ya madai kutoka kwa utawala mpya nchini Somlia unaoishutumuKenya kwa kuingilia masuala yake ya ndani na kuweka vizuizi mjini Kismayo.

Uganda  ina wanajeshi wengi  zaidi nchini Somalia pia wakiwemo wanajeshi kutoka Burundi, Kenya Sierra Leone,Djibouti na Somalia. Maafisa wanaohusika na masuala ya kigeni nchini Uganda wanasema kuwa mkutano huo ambao ni wa kwanza wa aina yake unataandaliwa kwenye eneo la starehe la Munyonyo.