Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaidizi wa Ban kutembelea Jamhuri ya Afrika ya Kati

Msaidizi wa Ban kutembelea Jamhuri ya Afrika ya Kati

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Ivan Šimonovic, anatazamia kuitembelea Jamhuri ya Afrika ya Kati kuanzia Julai 29 hadi August 2 mwaka huu.Kwenye ziara yake hiyo, Simonovic atakutana na viongozi wa serikali ya mpito akiwemo Waziri Mkuu, Mkuu wa serikali ya mpito, mashirika ya kiraia na jumuiya za kimataifa.

Msaidizi huyo wa Katibu Mkuu anatazamia pia kutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kufanya tathmini na baadaye kukutana na waandishi wa habari.

Pamoja na kutembelea mji mkuu Bangui, pia amepanga kutembelea miji mingine kama Bambari ulioko Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo