Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo ya chakula na utapia mlo yaendelea kuisakama Malawi:UM

Matatizo ya chakula na utapia mlo yaendelea kuisakama Malawi:UM

Sera za karibuni za Malawi kuhusu usalama wa chakula zimeshindwa kuliondoa taifa hilo kwenye tatizo sugu la ukosefu wa chakula na utapia mlo kwa mujibu wa mtalaamu huru wa haki za binadamu na haki ya chakula wa Umoja wa Mataifa. Grace Kaneiya na taarifa zaidi (RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wa Malawi wameendelea kusalia kwenye lindi la umaskini, na robo tatu yao wanatajwa kuwa katika hali mbaya . Wengi wao wanashindwa kugharamia mlo kamili kutokana na kuwa na kipato cha chini.

Hali hii imewaathiri watoto wengi kwani ripoti zinasema kuwa nusu ya watoto wanakabiliwa na matatizo ya utapiamlo.

Oliver Deshuter ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula

(CLIP YA OLIVER DESHUTER)