Washindi wa shindano la Uchina la uchoraji kuhusu mazingira kwa watoto wataja:UNEP

17 Julai 2013

Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa mataifa UNEP limesema watoto zaidi ya 630,000 wa shule wakiwa na brush na rangi za kuchorea wameshiriki shindano la mwaka huu la uchoraji lililobeba kauali mbiu Maji:yanatoka wapi? Na baada ya mchakato mzito Jumanne washindi wamepokea tuzo zao kwenye hafla maalumu iliyofanyika makao makuu ya UNEP mjini Nairobi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Baada ya sherehe hiyo watoto hao pamoja na walimu wao walizuru mbuga ya wanyamapori ya Maasai Mara na kushirirki kwenye shughuli ya uchoraji wakishirikiana na watoto wa shule kutoka sehemu ya mabanda ya Mathare iliyo mjini Nairobi. Shindano hilo la kuchora ni sehemu ya  mpango wa masomo kwa watoto kutoka China mpango ambao pia unaungwa mkono na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP.

Kama sehemu ya masomo kuhusu hamasisho  somo la mazingira limejumuishwa kwenye mfumo wa masomo ya shule nchini China. Mwaka huu zaidi ya watoto milioni 3 walishiriki kwenye mpango huo. Karibu walimu 50 pia wamepata mafunzo kuhusu mazingira na maendeleo endelevu.

Kila mwaka mpango wa elimu ya watoto kuhusu mazingira nchini China huandaa shindano la kuchora. Shindano hilo hulenga kuwachochea wasanii wachanga kuwa viongozi wa mazingira siku za baadaye.