Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Ethiopa waliokwama Yemen wamerejea nyumbani:IOM

Wahamiaji wa Ethiopa waliokwama Yemen wamerejea nyumbani:IOM

Kundi la watu 131 wahamiaji kutoka Ethiopia ambao walikwama nchini Yemen sasa wamefanikiwa kurejea nyumbani kwa hiari kwa usafiri wa ndege ya shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM.

Kuwasili kwa raia hao mjini Addis Ababa, kunafanya idadi jumla waliokwisha rejea nyumbani kufikia 765 tangu lilipoanza zoezi hilo Juni mwaka huu.

Zoezi la kuwarejesha wahamiaji hao nyumbani kwa hiari lilisimamishwa September mwaka jana kutokana na ukosefu wa fedha.

Lakini kupatikana kwa fedha kiasi cha dola za Marekani 260,000 kutoka kwa mfuko wa Umoja wa Mataifa unaohusika na majanga ya dharura kumeliwezesha shirika la kimataifa IOM kurejesha upya mpango huo.

Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM

 (SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)