Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel iondoe vikwazo vya kusafiri Gaza: OCHA

Israel iondoe vikwazo vya kusafiri Gaza: OCHA

Mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, James Rawley, ametoa wito kwa serikali ya Israel kuondoa vikwazo vya muda mrefu, ambavyo vimekuwepo kwenye ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007.Akitaka kumulika athari za vikwazo hivi kwa maisha ya watu, Bwana Rawlye aliongoza ziara ya ujumbe wa mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu na wawakilishi wa kimataifa kukutana na wavuvi wa Kipalestina na wakulima ili kujionea moja kwa moja jinsi wanavyoathiriwa na changamoto wanazokumbana nazo.

Bwana Rawlye amesema, kwa ujumla, vikwazo vya Israel vimeleta madhara makubwa kwa riziki za familia zilizopo Gaza, kama wavuvi na wakulima walokutana nao.

Amesema vikwazo hivyo vinawaathiri zaidi watu fukara, na kuzuia ukuaji wa uchumi endelevu, na hivyo kuwafanya waendelee kutegemea misaada. Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa asilimia 57 ya watu Gaza hawana fedha za kununua chakula cha kutosha, huku asilimia 80 ya familia zote zikitegemea misaada ya kimataifa.