Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unyanyapaa kikwazo cha kutokomeza Fistula : UNFPA

Unyanyapaa kikwazo cha kutokomeza Fistula : UNFPA

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza fistula, Shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA limezungumzia hali ilivyo nchiniTanzaniana kile inachofanya kutokomeza ugonjwa huo. Flora nducha na maelezo zaidi.(TAARIFA YA FLORA)

Shirika la idadi ya watu duniani, UNFP linasema nchiniTanzaniakila mwaka kuna wagonjwa wapya Elfu Tatu wa Fistula itokanayo na uzazi na kwamba tatizo hila limejikita zaidi ukanda wa Ziwa.

Naibu Mwakilishi wa UNFPA nchini humo Rutasha Fulgence ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa kati ya wagonjwa hao wapya ni Elfu Moja tu ndio wanaweza kupata tiba na kikwazo kikubwa ni unyanyapaa.

(Sauti ya Rutasha)

“Tatizo kuu la Fistula ni unyanyapaa na kutengwa na jamii ambayo hatimaye inasababisha  umaskini kwa kuwa huyu mwanamke hawezi tena kushiriki shughuli za uzalishaji. Na hizi ndio changamoto na athari zinazokuja na fistula ya uzazi. Unyanyapaa! Unyanyapaa! Ndio tatizo kuu la Fistula!”

Mwanaidi Abdallah, mkazi wa Morogoro mashariki mwaTanzaniaalipata Fistula baada ya kujifungua na mtoto wake alifariki dunia, hata hivyo yeye kupitia matangazo ya Radio aliweza kupata taarifa juu ya tiba ya Fistula na kwenda hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam.

(Sauti ya Mwanaidi)

Naye mkurugenzi mkuu wa UNFP Babatunde Osotimehin amesema shirikalakelinafanyamambo mbalimbali ili kuhakikisha wanatokomeza maradhi haya

 (SAUTI YA BABATUNDE)

"Tunatoa mafunzo kwa wauguzi wengi zaidi  na wahudumu wa afya karibu na mahali ambapo watu wanaishi, ili wasisafiri umbali mrefu kabla ya kupata huduma. Tunapendekeza kila mwanamke mwenye mimba kuhudhuria kliniki mara tatu au nne wakati wa ujauzito. Tumeona katika baadhi ya sehemu za Afrika naIndiaambako kuna maradhi haya , hatuhitaji kuwa na wakunga ambao wamesomasana. Kwa hakika ukitoa mafunzo kwa mtu mwenye ujuzi wa ukunga ambaye anaishi kwenye jamii karibu na watu wanaowahudumia unaweza kupunguza na kukaribia  kumaliza kabisa tatizo hili."