Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni mpya ya chanjo dhidi ya numonia yang'oa nanga

Kampeni mpya ya chanjo dhidi ya numonia yang'oa nanga

Nchini Uganda, ugonjwa wa numonia huua hadi watoto ishirini na nne elfu chini ya miaka mitano kila mwaka. Lakini sasa maelfu ya maisha ya watoto yataokolewa kufuatia kuanzisha chanjo mpya ya PCV dhidi ya ugonjwa huo.Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, na Shirika la Afya Duniani, WHO, kwa ushirikiano na serikali ya Uganda yalizindua kampeni hiyo ya chanjo, katika hafla ilohudhuriwa na rais Yoweri Museveni kama mgeni wa heshima

(SAUTI-RAIS MUSEVENI)

“Afya ni mali. Ikiwa afya ni mali, ni nini kinachohitajika ili kuhakikisha maisha yenye afya? Cha kwanza ni chanjo”

Chanjo ya PCV imewezeshwa kuwepo kutokana na ufadhili mkubwa kutoka kwa GAVI Alliance, ambao ni ushirika wa kimataifa wa afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto kwa kuwapa chanjo. Dr. Seth Berkley ni Mkurugenzi Mkuu wa GAVI Alliance

(SAUTI - Dr. Seth Berkley, GAVI Alliance)

“Numonia sasa inaongoza kuwa sababu ya vifo vya watoto inayoweza kuzuiliwa. Hapa Uganda, takriban asilimia 17 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano hutokana na numonia, na asilimia kubwa ya vifo hivyo husababishwa na baktiria aina ya pneumococcal, kwa hiyo chanjo ya PCV in uwezo wa kuzuia vyote hivyo.”

Chanjo ya PCV pia huzuia ugonjwa wa meningitis, ambao pia ni hatari kwa maisha, na inatarajiwa kuwafikia hadi watoto milioni 1.4 nchini Uganda mwaka huu pekee.

Kuanzisha chanjo ya PCV nchini Uganda ni hatua kubwa katika kufikia lengo la milenia la kupunguza vifo vya watoto kwa thuluthi mbili ifikapo mwaka 2015.

(MAKALA SAUTI-MMALI)