Kuharibiwa kwa maeneo wanayopumzikia ndege wanahoama kunaharatisha familia nyingi za ndege:UNEP

10 Mei 2013

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP linasema kuwa tukio la kuhama kwa ndege kila mwaka ambapo karibu ndege milioni 50 wanahama ikiwa ni karibu asilimia 19 ya familia 10,000 ya ndege duniani ni moja ya maajabu makubwa duniani lakini hata hivyo maeneo ambayo ndege hawa hutumia kukamilisha safari zao yameharibiwa au yanatoweka kabisa. Alice Kariuki anaripoti.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Maeneo haya yaliyo hatari ndiyo ndege wanaohama hupumzika , huzaa na kula wakati wa msimu wao wa kuhama. Kutokana na kuharibika kwa maeneo hayo familia fulani ya ndege huenda ikatoweka kwa kipindi cha miaka kumi inayokuja huku jamii zingine zikitarajiwa kuwapoteza ndege wengi hata hadi asilimi tisa kila mwaka. Siku ya kuhama kwa ndege duniani ikiwa inasherekewa kati ya tarehe 11-12 mwezi Mei, maadhimishao ya mwaka huu yataangazia umuhimu wa maeneo haya katika kuendelea kuishi kwa ndege hawa, hatari ndege wanaohama wanakabiliana nayo na sababu ya kutaka kuwepo ushirikiano wa kimataifa kulinda maeneo hayo. Kati ya yale yanayotarajiwa siku hiyo ni mafunzo, kuonyeshwa kwa filamu na safari za kutazama ndege. Katibu mkuu wa Umoja Ban Ki moon anasema kuwa anaunga mkono kampeni ya kuhamasisha kuhusu hatari zinazowakumba ndege wanaohama na kutoa wito kwa jitihada kufanywa kulinda ndege wanaohama.