Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria hayajathibitishwa:UM

Madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria hayajathibitishwa:UM

Tume huru ya kimataifa inayochunguza Syria imetoa ufafanuzi kwamba uchunguzi wake haujapata uthibitisho kamili kuhusu madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria.Tume hiyo huru kutoka baraza la haki za binadamu imesema sio serikali wala upande wa upinzani ambao wamebainika kutumia silaha hizo, na kwa hivyo haiko katika nafasi ya kutoa matamshi yoyote zaidi kuhusu madai hayo kwa sasa.

Mwenyekiti wa tume hiyo Paulo Sergio Pinheiro amezikumbusha pande zote kwenye mgogoro wa Syria kwamba matumizi ya seilaha za kemikali ni marufuku kwa mazingira yoyote yale chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.