Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto nchini Somalia kupewa chanjo dhidi ya magonjwa matano hatari

Watoto nchini Somalia kupewa chanjo dhidi ya magonjwa matano hatari

Karibu watoto 500,000 wanaozaliwa nchini Somaliakila mwaka watanufaika na chanjo mpya ya kuwakinga dhidi ya magonjwa matano yaliyo hatari kwa maisha ya watoto. Jason Nyakundi ameandaa taarifa hii.

(PKG YA JASON NYAKUNDI)

Chanjo hiyo itawakinga watoto dhidi ya magonjwa kama dondakoo, pepo punda, kifaduro , Hepatitis B na Haemophilus influenza ambayo ni bacteria inayosababisha magonjwa ya uti wa mgongo na pneumonia.

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa mzozo unaondelea nchiniSomalia umevuruga mfumo wa afya na kuchangia taifa hilo kuwa na huduma mbaya zaidi za kiafya duniani.

Shirika hilo linasema kuwa mmoja kati ya watoto watano nchini Somali hupoteza maisha kabla ya kuhitimu umri wa miaka mitano.

Mjumbe wa UNICEF nchini Somalia Sikander Khan anasema kuwa chanjo hiyo mpya itasaidia  kuzuia vifo vya watoto nchini Somalia.

 (SAUTI YA SIKANDER KHAN)

"Ninaaamini kwa dhati kuwa tutaleta mabadilko na tutaondoa dhana ambayo imekuwepo katika nchi hii kwa watoto kwa muda wa miaka 20 na ziaidi”

UNICEF , Shirika la Afya Duniani WHO na lile la Gavi Alliance zinatoa zaidi ya chanjo milioni 1.3 nchini Somalia mwaka huu ambapo kila mtoto atakuwa akipewa chanjo tatu.