Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua kampeni ya changamoto ya kutokomeza njaa Asia-Pacific

UM wazindua kampeni ya changamoto ya kutokomeza njaa Asia-Pacific

Umoja wa mataifa Jumatatu umezindua kampeni ya changamoto ya kutokomeza njaa kwenye ukanda wa Asia na Pacific. Alice Kariuki na taarifa zaidi(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Kamepeni hiyo iliyozinduliwa mjini Bangkok Thailand na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa ukanda huo inazitaka serikali, wakulima, wanasayansi, wafanya biashara,jumuiya za kijamii na walaji kushirikiana kutokomeza tatizo la njaa katika ukanda huo ambako asilimia kubwa ya watu ni masikini.

Akizungumza katika uzinduzi huo naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema dunia haiwezi kupumzika wakati watu wengi sana duniani walala njaa na kukabiliwa na matatizo mengi yanayotishia malengo ya maendeleo ya milenia.

(SAUTI YA JAN ELIASSON)