Skip to main content

WHO yaongoza mikakati ya kupambana na ugonjwa wa surua nchini Cambodia

WHO yaongoza mikakati ya kupambana na ugonjwa wa surua nchini Cambodia

Taifa la Cambodia limeongeza maradufu idadi ya watoto wanaopata chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua kwa muda wa miaka kumi iliyopita.

Hadi mwaka 2011 asilimia 20 ya watoto wote nchini Cambodia hawakuwa wanapata chanjo wanayohitajika ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa surua. Mwaka 2011 shirika la afya duniani WHO lilitoa mchango kwa programu ya kitaifa ya Cambodoa katika kutoa kampeni ya nchi nzima kuchunguza hali ya chanjo kwa wanawake na watoto na kubaini jamii zilizo kwenye hatari ikiwa zitakosa chanjo.

Ikiwa watoto hawapelekwi kwenye vituo vya afya kupewa chanjo ina maana kuwa programu hiyo ingetafua njia za kuwafikia watoto hao. Programu hiyo iligundua kuwa kulikuwa na jamii 1600 ambazo watoto hawakuwa wanapata chanjo ambapo ilipanga mikakati wa kuwapa chanjo kupitia kwa wahudumu wa kujitolea wa afya.