Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya UM ya kulipa fidia yailipa Kuwait dola bilioni 1.13

Tume ya UM ya kulipa fidia yailipa Kuwait dola bilioni 1.13

Tume ya Umoja wa mataifa ya fidia leo imetoa dola bilioni 1.13 kwa ajili ya kuilipa Kuwait ikiwa ni sehemu ya madai yaliyosalia ya nchi hiyo.Kwa malipo hayo tume sasa itakuwa imeshalipa dola bilioni 41.2 ya jumla ya dola bilioni 52.4 ilizoahidi kwa mataifa zaidi ya 100 na mashirika ya kimataifa kufuatia madai zaidi ya milioni 1.5 yaliyowasilishwa. Baada ya malipo hayo sasa tume hiyo itasalia na dola bilioni 11.2 za kulipa.

Madai yaliyosalia yaliwasilishwa na serikali ya Kuwait kwa niaba ya shirika la petrol la Kuwait, na mwaka 2000 iliahidiwa kulipwa dola bilioni 14.7 kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta na hasara ya mauzo iliyopata kutokana na athat za rasilimali za mafuta za Kuwait.

Fedha hizo ni sehemu kubwa kabisa ya fedha ambazo zimewahi kutolewa na tume ya fidia ya UM kwa nchi moja.