Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaweza kushinda vita dhidi ya Malaria Global Fund

Tunaweza kushinda vita dhidi ya Malaria Global Fund

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria yaani Global Fund umesema leo kwamba hatua mpya katika upande wa kisayansi na utekelezaji wake vimetoa fursa kwa jamii ya kimataifa kudhibiti malaria na kuiondoa katika orodha ya maradhi tishio katika afya ya dunia.

Wakati mataifa mengi yakiadhimisha siku ya afya duniani hapo kesho Global Fund inasema kujidhatiti kwa wadau wote kunahitajika katika vita dhidi ya malaria ili kuzidisha juhudi ili kubadilisha maradhi hayo kutoka ugonjwa unaouwa zaidi kuwa ugonjwa unaoweza kukingwa na kutibika.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa Global Fund Mark Dybul dunia inaweza kushinda vita dhidi ya malariakamaitafanya kazi pamoja.Ameongeza kuwa kuna fursa kubwa ya kudhibiti na kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watoto wanaokufa kwa malaria kila mwaka.

Na endapo hatua hazitochukuliwa mapema amesema dunia itakuwa ikihesabu gharama za maradhi hayo kwa vizazi hadi vizazi.

Hatua zilizopigwa katika muongo uliopita dhidi ya malaria zimechangiwa na mabadadiliko ya kisayansi kama kunyuniza dawa katika vyandarua, upimaji wa haraka na dawa za kukinga malaria.

Miradi inayofadhiliwa na Global fund imesaidia usambazaji wa vyandarua zaidi ya milioni 30, upimaji rahisi wa malaria na matibabu kwa kutumia dawa mseto kama artemisinin. Mapema mwezi huu Global Fund ilitangaza kutaka kuchangisha dola bilioni 15 kwa kipindi cha mwaka 2014-2016 katika juhudi zake