Mkutano wa UN Habitat wahimitishwa

19 Aprili 2013

Mkutano wa 24 ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili unaohusisha uongozi wa Baraza la Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi , UN Habitat , umemalizika mjini Nairobi Kenya, kwa makubaliano juu ya ukuaji endelevu wa miji na umuhimu wa jukumu la shirika hilo kwa Umoja wa Mataifa. Mkutano huo wa siku tano pia umeangazia jukumu la miji katika kuunda fursa za kiuchumi kwa wote ikigusia vijana na jinsia.

Miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa ni kuunga mkono maandalizi ya kongamano la tatu la UNHABITAT litakalofanyika mwaka 2016 ambapo ajenda mpya ya kimataifa kuhusu miji itaundwa.

Nchi zaidi ya 1000 zimeshiriki katika mkutano huo kwa kuwakilishwa na zaidi ya wawakilishi mia moja ambao pia waliwakilisha sekta binafsi , asasi za kiraia , na vyombo vya habari.