Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama za kusafirishwa zaanzishwa kwenye kambi ya wakimbizi Uganda: UNHCR

Mahakama za kusafirishwa zaanzishwa kwenye kambi ya wakimbizi Uganda: UNHCR

Nchini Uganda, mfumo wa mahakama za kusafirishwa umeanza kujaribiwa mnamo Jumatatu Aprili 15 ili kurahisisha uwepo wa haki kwa wakimbizi ambao wamekosewa.Mradi huo unaoendeshwa kwenye kambi ya Nakivale kusini magharibi mwa nchi, umeanziswha na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kwa ushirikiano na serikali yaUganda.

Unatarajiwa kuwahudumia takriban wakimbizi 68,000 na raia wa Uganda 35,000 kwa kutoa huduma za haraka za kisheria.

Mfumo huu ndio wa kwanza kabisa kuwahi kuanzishwa nchiniUganda. George Njogopa na maelezo zaidi

(SAUTI YA GEORGE)