IOM na Panasonic kuukabili ukatili wa kijinsia Somalia kwa taa za nishati ya jua

9 Aprili 2013

Je, ukatili wa nyumbani unaweza kukabiliwa kwa kutumia taa zinazotumia nishati ya miale ya jua? Hili ndilo linajaribiwa kutekelezwa sasa hivi nchini Somalia na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji likishirikiana na kampuni ya Kijapan ya Panasonic, kama anavyoarifu Joseph Msami

(SAUTI MSAMI)

Katika kupambana na ukatili wa kijinsia nchini Somalia, Shirika la kimataifa la masuala ya umeme la nchini Japan, Panasonic, kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM,  limeanzisha utafiti wa namna taa za kutumia nishati ya miale ya jua zinavyoweza kupunguza ukatili huo katika kambi za wakimbizi na wahamiaji .

Mchango huo wa kiasi cha dola za Marekani elfu 31 unafuatia uchunguzi usio rasmi  wa IOM wa mwaka 2012 ulioonyesha  kuwa asilimia kubwa ya vitendo vya ukatili ikiwamo ubakaji hufanyika usiku katika makambi wakati kukiwa na giza .

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM na anaeleza namna utafiti huo utakavyofanyika.

(SAUTI JUMBE)