Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyandarua vyenye viuatilifu vyachochea uzalishaji wa maziwa: FAO

Vyandarua vyenye viuatilifu vyachochea uzalishaji wa maziwa: FAO

Njia rahisi na ya ubunifu ya kutumia madawa kwenye vyandarua kulinda mifugo kumeongeza mara mbili au mara tatu katika baadhi ya sehemu uzalishaji wa maziwa kwa wafugaji wadogowadogo, huku kukisaidia pia kupunguza maradhi yatokanayo na mbu kwa binadamu kwenye maeneo ya Kisii nchini Kenya limesema shirika la chakula na kilimo FAO.

Hayo yamebainika katika mradi maalumu wa shirika hilo ambao ni sehemu ya mkakati wa kuboresha afya ya mifugo katika maeneo mengi yanayoathirika na magonjwa ya maeneo ya joto.

Vyandarua vinavyotumika kwa mujibu wa FAO ni salama kwa mazingira na vimesaidia kwa takribani asilimia 90 kupunguza wadudu kama mbun'go , mbu na waududu wengine wanaosababisha majongwa.

Pia vimesaidia kuongeza masuala ya usafi wakati wa ukamuaji maziwa na kuwaelimisha wafugani jinsi ya kupunguza magonjwa kwa mifugo yao. George njogopa na taarifa kamili.