Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yapambana na waasi DRC Kongo,juhudi zaidi zahitajika

MONUSCO yapambana na waasi DRC Kongo,juhudi zaidi zahitajika

Kongo DRC ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika yenye rasilimali nyingi, ikiwemo madini na uoto wa asili. Nchi hii yenye idadi ya zaidi ya watu milioni sabini ina historia ndefu ya mapigano yaliyosababisha maafa kadhaa ikiwamo vifo, ulemavu na hata wakimbizi wa ndani ya nchi na wale waliokimbilia nchi jirani kutafuta hifadhi.

Mwishoni mwa mwezi February umeripotiwa mapigano katika kijiji cha Kitchanga kati ya kundi la Wanamgambo linalofahamika kama Muungano wa Wazalendo kwa ajili ya Kongo iliyo huru na inayojitegemea (APCL) na jeshi la serikali ya Kongo DRC (FARDC).

Mamia ya wakazi wa eneo wanajihifadhi katika kambi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa iliyoko chini ya Umoja wa Afrika AU ili kupata malazi. Joseph Msami anasimulia zaidi katika makala hii ianyomulika namna Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wanavyojitahidi kutuliza ghasia nchini Kongo DRC kwa kushirikiana na majeshi ya serikali.