Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yatoa mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa polisi wa kike

UNMISS yatoa mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa polisi wa kike

Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya wanawake Machi Nane ambapo tumeshuhudia maadhimisho hayo yakifanyika kwa matukio mbalimbali ikiwemo matembezi na kadhalika, nchini Sudan Kusini,Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, umetumia maadhimisho ya siku ya wanawake kwa kufundisha  Kiingereza  wanawake zaidi ya 50.  Mafunzo hayo yanafanyika katika hema lililoko katika karakana iliyoko katika kituo cha polisi Sudan Kusini ambapo askari wanawake wanaofundishwa lugha ya Kiingereza iliyo miongoni mwa lugha rasmi ya nchi  ni kutoka Jeshi la Polisi la nchi hiyo.Ungana na Joseph Msami katika makala hii inayojikita katika juhudi za Ujumbe wa  Umoja wa Mataifa nchini Sudan katika kusaidia kutoa elimu kwa askari polisi wa kike.