Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi wa serikali DRC walotekeleza uhalifu waadhibiwe: MONUSCO

Wanajeshi wa serikali DRC walotekeleza uhalifu waadhibiwe: MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUSCO), umesema kwamba umepokea maelezo yanayoonyesha kuhusika kwa vikosi vya serikali (FARDC) katika vitendo vya ubakaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu mnamo mwezi Novemba mwaka 2012.

Maelezo haya yametokana na uchunguzi ulofanywa na ujumbe wa haki za binadamu kwenye mji wa Minova na vijiji jirani kwenye mkoa wa Kivu ya Kaskazini kati ya Disemba 2012 na Februari 2013.

Mnamo Februrari tarehe 4 2013, MONUSCO ilituma barua kwa kamanda mkuu wa FARDC ikimwomba avipumzishe vikosi husika kutoka kwa majukumu yao, na kutuma waraka mwingine mnamo tarehe 18 February kutaka  kamanda mkuu wa jeshi atomize matakwa hayo.

MONUSCO imesemea bado inazitolea mwito mamlaka za uongozi wa DRC kwenye ngazi za juu ili kuhakikisha ya kwamba washukiwa wote wanafikishwa mbele ya mkono wa sheria, na kwamba itaendelea kusaidia vyombo vya sheria katika DRC kuendelea kufanya uchunguzi, na kuwahukumu washukiwa.