Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yajiandaa kutoa misaada ya kibinadamu kabla ya uchaguzi wa Kenya

IOM yajiandaa kutoa misaada ya kibinadamu kabla ya uchaguzi wa Kenya

 Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesema linaweka mikakati ya kujiandaa kutoa misaada ya kibinadamu nchini Kenya, siku chache kabla ya uchaguzi nchini humo hapo Jumatatu.

Shirika hilo limesema linashirikiana na serikali kuweka mipango ya dharura ambayo itajumuisha sekta mbali mbali, ili kuwa tayari kwa uchaguzi huo, kwa kuandaa bidhaa zisizo chakula.

IOM pia imetambua mashirika ambayo yana uwezo wa kushirikiana nayo, pamoja na kufanya warsha za mafunzo katika utoaji wa miaada ya dharura kwa wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

SAUTI YA JUMBE