Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa UM kuhusu vifungo vinavyokiuka haki wakamilisha ziara Ugiriki

Wataalam wa UM kuhusu vifungo vinavyokiuka haki wakamilisha ziara Ugiriki

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu vifungo vinavyokiuka haki za binadamu limekamilisha ziara yake nchini Ugiriki, ambayo ilitekelezwa kwa lengo la kukagua hali ya watu kunyimwa haki zao nchini humo.

Kundi hilo la wataalam huru lililoteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu, lilizuru vituo kadhaa vya kuzuilia watu, zikiwemo jela, vituo vya polisi, vituo vya kuwazuilia wahamiaji na vituo vya watu wenye matatizo ya akili.