Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa UM watembelea kambi ya Auschwitz-Birkenau

Maafisa wa UM watembelea kambi ya Auschwitz-Birkenau

Kundi la watu mashuhuri na waakilishi kutoka nchi 40 wameungana kwenye shughuli inayoongozwa na Umoja wa Mataifa ya kutembelea kambi ya mauaji ya manazi ya Auschwitz-Birkenau nchini Poland shughuli ambayo inaongozwa na mkurugenzi wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova .

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro akiandamana naye Bokova alihudhuria makumbusho ya waathiriwa wa kambi hiyo ambapo zaidi ya watu milioni moja wengi wao wayahudi waliuawa. Kukombolewa kwa kambi hiyo mnamo tarehe 27 mwezi Januari mwaka 1945 sasa kunatambuliwa kama siku ya kimataifa ya kuwakumbuKa wathiriwa ka kambi hiyo.

 Kambi ya Auschwitz-Birkenau pia iliorodheshwa mwaka 1979 kama moja ya maeneo ya kitamaduni duniani.