Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yajiandaa kuwasaidia walio na nia ya kurejea makwao nchini Mali

UNHCR yajiandaa kuwasaidia walio na nia ya kurejea makwao nchini Mali

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa linajianda kuwasaidia wale waliohama makwao kaskazini mwa nchi na walio na nia ya kurejea kwa hiari wakati hali inapoendelea kubadilika nchini Mali.

UNHCR inasema kuwa ina mpango wa kufungua ofisi zake mjini Gao na kwenye miji mingine eneo la kaskazini hivi karibuni hata kama hali mbaya ya usalama imekuwa ikitatiza utoaji huduma eneo la kaskazini.

Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa kulingana na maoni kutoka kwa wale waliohama makawao siku chache zilizizopta kuna dalili kuwa wana nia ya kurudi makwao.

(SAUTI YA ADRIAN)

UNHCR inatoa wito kwa viongozi wa jamii na utawala wa Mali kuangazia zaidi yale yanayoweza kuleta uwiano na amani kati ya jamii.