Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay ataka majadiliano ya dhati Misri ili kuepusha maafa zaidi

Pillay ataka majadiliano ya dhati Misri ili kuepusha maafa zaidi

Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navyi Pillay amesema kumekuwa na hali ya wasiwasi kufuatia kuongezeka kwa matukio ya mauaji ya watu na kushamiri kwa vurugu kunakoshuhudiwa sasa nchini Misri na amezita pande zote kuanzisha majadiliano ili kuondokana na hali hiyo.

Pia Pillay ameitolea wito serikali ya Misri kutafakari upya njia zake inazochukua ikiwemo utumiaji wa nguvu kupita kiasi kukabili maandamano yanayoendeshwa na wananchi waliochukizwa na mwenendo wa Rais Mohamed Mursi. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)