Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani yatoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa Global Fund

Ujerumani yatoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa Global Fund

Jamhuri ya Ujerumani imetoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa kimataifa wa kupiga vita UKIMWI, kifua kikuu na malaria, yaani Global Fund, ili kuwasaidia wahudumu wa afya kuendeleza juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa haya hatari ya kuambukiza.

Tangazo la mchango huo limetolewa leo na Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dirk Niebel, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Davos, Uswisi, ambako mkutano wa kimataifa kuhusu uchumi unaendelea. Miongoni mwa waliokuwepo wakati wa tangazo hilo ni mkwasi wa Microsoft Bill Gates na Mkurugenzi Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul.