Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola 20 kila mwezi zitolewazo na UNICEF kwa kaya maskini nchini Kenya zabadili maisha

Dola 20 kila mwezi zitolewazo na UNICEF kwa kaya maskini nchini Kenya zabadili maisha

Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kutoa msaada kidogo wa fedha kwa jamii maskini katika nchi zinazoendelea ili kujikwamua kutoka lindi la umaskini umeanza kuzaa matunda na kubadili maisha ya jamii hizo ikiwemo nchini Kenya.

Chini ya mpango huo, UNICEF hutoa dola Ishirini kila mwezi kwa mtu aliyejiandikisha ambapo mhusika hutumia fedha hizo kwa shughuli mbali mbali ikiwemo miradi ya biashara na hata kulipa ada za matibabu na shule.

Mmoja wa wanufaika hao, Caroline Adhiambo Mula amesema kupitia mradi huo unaofadhiliwa na UNICEF na kuendeshwa na serikali ya Kenya umemwezesha kulipa karo za shule, ada za matibabu ya kufungua sehemu ya urembo kwa nywele za wanawake na ana matarajio zaidi.

(SAUTI YA CAROLINE MBUGUA)

Naomi Mbugua afisa anayehusika na watoto katika serikali ya Kenya amesema mpango huo ni muhimu hususan kwa mayatima na makundi mengine ya watu walio katika mazingira magumu ambapo kwenye eneo la Dagoretti wanasaidia kaya 657.