Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kasi ya kukabili tatizo la Malaria imepungua: WHO

Kasi ya kukabili tatizo la Malaria imepungua: WHO

Shirika la Afya duniani WHO, limechapisha ripoti yake ya mwaka 2012 inayoaangazia tatizo la Malaria ambayo imesema kasi ya kukabiliana na tatizo hilo imekosa msukumo na kushuka kiasi.

Ripoti hiyo ambayo imezinduliwa katika mji Mkuu wa Liberia, Monrovia na rais wa taifa hilo, Ellen Johnson Sirleaf, imeonyesha kushuka kwa jitihada za kukabiliana na kasi ya ugonjwa huo. Imesema kuwa wakati harakati za kudhibiti ugonjwa huo ilipata msukumo mkubwa katika kipindi cha mwaka 2004 na 2009, lakini mwamko huo ulishuka katika kipindi cha mwaka 2010 na 2012. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)