Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Umoja wa Mataifa laongeza muda wa kuhudumu kwa majaji kwenye mahakama ya ICTR

Baraza la Umoja wa Mataifa laongeza muda wa kuhudumu kwa majaji kwenye mahakama ya ICTR

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu kwa majaji watano kwenye mahakama ya kimataifa inayosikiliza kesi za uhalifu wa kivita nchini Rwanda ICTR kwa lengo la kuiwezesha mahakama hiyo kumaliza kazi yake. Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Arusha nchini Tanzania ilibuniwa baada ya kutokea mauaji ya halaiki nchini Rwanda ambapo watu 800,000 wengi kutoka kabila la Watusi waliuawa mwaka 1994 mauaji yaliyodumu kwa muda wa miezi mitatu. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi: