Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna viwanda vya nyuklia Japan shwari kufuatia tetemeko la ardhi: IAEA

Hakuna viwanda vya nyuklia Japan shwari kufuatia tetemeko la ardhi: IAEA

Idara ya mikasa na masuala ya dharura ya Shirika la Kimataifa la Atomiki, IAEA, imesema inawasiliana na mamlaka husika nchini Japan kufuatia tetemeko la ardhi lililopima kiwango cha 7.3 kwenye chombo cha kupima ukubwa wa tetemeko la ardhi.

IAEA imesema viwanda vya nguvu za nyuklia katika maeneo ya karibu na uti wa tetemeko hilo vimeripoti kwa hamashauri ya kitaifa ya nyuklia nchini Japan (NRA) kuwa havikutambua matatizo yoyote, na kwamba hakuna tahadhari za dharura zilizotangazwa.

Ripoti ya NRA, ambayo ilitolewa kupitia mfumo wa kubadilishana habari za mikasa na tahadhari (USIE), imesambazwa kwa mataifa wanachama wa IAEA na mashirika ya kimataifa. Kama sehemu ya taratibu zake, IAEA imesema ipo tayari kuisaidia Japana kwa lolote ikiwa msaada wake utahitajika.