Upatikanaji wa chakula, uwezo wa kipato, changamoto kuu zinazokabili Haiti

13 Novemba 2012

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema kuwa zaidi ya raia milioni 1.5 wa Haiti wapo hatarini kukubwa na tatizo la ukosefu wa chakula na limetaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukwamua kadhia hiyo.

Shirika hilo limesema kuwa hali iliyojitokeza hivi karibuni ya mabadiliko ya hali ya hewa iliyoenda na ukame wa mvua inaweza kusababisha kiasi hicho cha watu wakakubwa na baa la njaa ifikapo mwaka 2013.

Mkurugenzi wa WFP nchini Haiti Myrta Kaulard amesema wasiwasi mkubwa unaojitokeza sasa ni kuhusu maeneo yaliyokumbwa na kimbunga Sandy ambayo hadi wakati huu bado hajafikiwa na mkakati wowote.

Pamoja na mikwamo mingine ya kijiographia lakini maeneo mengi nchini humo yameharibiwa na wakati huu yanazidi kukabiliwa na wasiwasi wa kukumbwa na uhawa wa chakula kutokana na kukosekana mvua za kutosha. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA ELIZABETH BRYS)