Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya “Mimi pia ni mhamiaji” yaanzishwa Afrika Kusini: IOM

Kampeni ya “Mimi pia ni mhamiaji” yaanzishwa Afrika Kusini: IOM

Nchini Afrika kusini, Shirika la Uhamiaji la kimataifa, IOM kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wanaanzisha kampeni iitwayo, Mimi pia ni mhamiaji yenye lengo la kuhamasisha raia wa nchi hiyo wafahamu kuwa wahamiaji nao pia ni sehemu ya jamii yao na hivyo kuleta utangamano miongoni mwa wakazi wote.

Kampeni hiyo itaendelea hadi tarehe 18 mwezi ujao ambayo ni siku ya kimataifa ya wahamiaji, ikijikita zaidi kuelimisha kuwa kimsingi raia wote wa Afrika Kusini ni wahamiaji au wana uhusiano na wahamiaji.

Tayari IOM imemteua Stoan Seate , mmoja wa wasanii bora nchini Afrika Kusini na mtu mashuhuri kuwa balozi wa kampeni hiyo ambapo msanii huyo amekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya chuki dhidi ya wahamiaji. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM:

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)