Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kutokomeza polio haziwafikii walio hatarini zaidi: WHO

Juhudi za kutokomeza polio haziwafikii walio hatarini zaidi: WHO

Ugonjwa wa kupooza, yaani polio, hautatokomezwa nchini Pakistan pasi mpango wa kitaifa kuwafikia wazazi kutoka makundi ya jamii ambayo yamo hatarini zaidi, kama vile jamii za kipato cha chini za Pashtun, ambazo huathiriwa zaidi na ugonjwa huo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliyochapishwa kwenye taarifa ya habari ya Shirika la Afya Duniani, WHO ya mwezi huu.

Utafiti huo uliwafuatilia wazazi 1017 wa watoto chini ya miaka mitano katika eneo la Karachi, kati ya Septemba na Oktoba mwaka uliopita. Utafiti huo ulitambua kuwa asilimia 41 (412) ya watu hao walisema hawajawahi kusikia lolote kuhusu polio, huku asilimia 11.4 (116) wakisema walikataa watoto wao wasipewe chanjo.

George Njogopa na Taarifa kamili