Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya wakulima muhimu katika kuulisha ulimwengu: FAO

Mashirika ya wakulima muhimu katika kuulisha ulimwengu: FAO

Shirika la chakula na kilimo, FAO, limesema mashirika ya wakulima, ambayo tayari yanawahusisha mamilioni ya wakulima wadogo, yanaweza kupanuliwa na kuchangia kwa kiasi kikubwa hata zaidi katika kukabiliana na umaskini na njaa, iwapo yataungwa mkono ipasavyo na serikali, mashirika ya umma na wasomi.

Kauli hii imetolewa katika kuadhimisha siku ya chakula duniani leo, ambayo inasherehekewa katika nchi 150, chini ya kauli mbiu: “Mashirika ya wakulima- muhimu kwa kuulisha ulimwengu”.

Katika ujumbe wake, Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jose Graziano da Silva, amesema ni muhimu kuboresha udhibiti wa usalama wa chakula kwenye ngazi ya kimataifa, ili kukabiliana vyema na mfumko wa bei ya chakula uliopo sasa duniani. Amesema hatua muhimu tayari zimepigwa katika masuala ya uongozi, hasa katika kuunda kamati inayohusiana na usalama wa chakula, CFS. Amesema ulimwengu unahitajika kuwa na mtazamo wa mbele kuelekea katika kuiangamiza kabisa njaa.

(SAUTI YA GRAZIANO da SILVA)