Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa haki za binadamu wakutana mjini Yamoussoukro

Wataalamu wa haki za binadamu wakutana mjini Yamoussoukro

Watalaamu wa tajriba ya juu kutoka kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa na tume ya Afrika ya kibinadamu na haki za watu wameahidi kuungana katika kupigania haki za binadamu barani Afrika. Akihutubia mkutano wa wawakilishi wa mataifa ya Afrika , mashirika ya umma waliokusanyika mjini Yamoussoukro nchini Ivory Cost mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yanayofanywa kinyume na sheria, Christof Heyns amesema kuwa umoja ni muhimu kwenye jitihada za kupigania haki za binadamu. Jason Nyakundi na Taarifa Kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)