Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya dola milioni 38 zahitajika kwa misaada ya kibinadam nchini Lesotho: UM

Zaidi ya dola milioni 38 zahitajika kwa misaada ya kibinadam nchini Lesotho: UM

Zaidi ya dola milioni 38 zinahitajika kwa dharura kufadhili huduma za kibinadamu nchini Lesotho, kwa mujibu wa ombi lilotangazwa leo na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadam. Kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula, WFP, fedha hizo zitayasaidia mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine kutoa misaada ya kibinadam kwa takriban watu 118, 000, ambao wameathirika zaidi. Misaada zaidi ya muda mrefu itahitajika kwa wengine 725, 000, ambao wana uhaba wa chakula, kama vile kuweka mipango ya kuboresha uzalishaji wa kilimo, afya na lishe.

Taifa la Lesotho linakabiliwa na tatizo la njaa ambalo limesababishwa na misimu miwili ya ukame hivi karibuni, na mvua nzito na mafuriko yaloharibu mimea kabla ya ukame huo. Mnamo tarehe 9 Agosti mwaka huu, Waziri Mkuu wa Lesotho alitangaza hali ya dharura ya uhaba wa chakula, na serikali yake kutoa ombi la msaada wa kibinadam kutoka kwa jamii ya kimataifa. Elisabeth Brys ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA ELIZABETH BRYS)