Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali

Ban afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amefanya mkutano na Waziri mkuu wa Somalia bwana Abdiweli Ali ambapo amempongeza kutokana na hatua za kisissa ambazo zimepigwa nchini Somalia kupitia kumalizika kkwa kipindi cha mpito.

Wakati wa wa mkutano huo wawili hao walijadili hatua za kisiasa na za kiusalama zilizopigwa nchini Somalia na umuhimu wa kuunga mkono udhabiti na ujenzi wa taasisi miezi inayokuja. Pia walizungumzia suala la kuendelea kuwepo msaada wa Umoja wa Mataifa kwenda Somalia hasa msaada ya kufadhili mikakati ya amani , kwenye masusla ya haki ya binadamu na suala la uharamia.