Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakalimali wa UM wasaidia kuchangisha fedha kuwasaidia wakimbizi wa Syria

Wakalimali wa UM wasaidia kuchangisha fedha kuwasaidia wakimbizi wa Syria

Wakalimali wa lugha ya Kiarabu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, wamechangisha dola 12, 000 kupiga jeki operesheni za Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR za kutoa misaada ya dharura kwa maelfu ya wakimbizi wa Syria.

Mkurugenzi wa ofisi ya kuratibu masuala ya shirika la UNHCR mjini New York, Udo Janz, amesema kuwa mchango huo utakuwa muhimu na kubadili hali ya wakimbizi wengi wa Syria, ambao wanahitaji usalama na misaada ya dharura.

Hali nchini Syria imekuwa ya kutia wasiwasi kote duniani na hasa kwenye makao makuu ya UMoja wa Mataifa, ambako ripoti zinaandaliwa kila siku kuhusu hali tete ya kibinadamam na kisiasa katika taifa hilo la Mashariki ya Kati. Wakalimali hao husoma ripoti hizi na kuzitafsiri kila siku, na wamesikitishwa na hali ilivyo, ndio maana wakaamua kuchangisha pesa kusaidia.