Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia wakati wa maandamano hazilindwi na sheria ya kimataifa ya haki za kibinadamu:UM

Ghasia wakati wa maandamano hazilindwi na sheria ya kimataifa ya haki za kibinadamu:UM

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kufanya maandamano na mikutano ya amani, Maina Kiai, amelaani ghasia ambazo zimekuwa zikiendeshwa kwenye mitaa ya miji kadha wa kadha duniani ya kupinga filamu ya kudhihaki Uislamu, akionya kuwa maandamano na mikutano ya hadhara ni lazima iwe ya amani ili ilindwe na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Amesema haki ya kufanya mikutano ya amani haitakiwi kuchukuliwa kama sababu ya kufanya ghasia. Bwana Kiai amesema kuwa kupaaza sauti au kutofurahia kitu kama hicho ni muhimu, lakini ni lazima kuheshimu haki ya kufanya mikutano ya amani. Amesema kuwa mauaji ya watu wasio na hatia, kama yaliyotendeka mashariki mwa Libya na uharibifu wa mali za watu ni vitu ambavyo haviwezi kukubalika kabisa. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)