Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yatangaza mpango wa kuimarisha usalama wawafanyakazi katika viwanda vya Pakistan

ILO yatangaza mpango wa kuimarisha usalama wawafanyakazi katika viwanda vya Pakistan

Shirika la Kimataifa la Ajira ILO, limetangaza kujitolea kwake kuzisaidia familia za wahanga wa moto ulotokea katika kiwanda cha nguo mjini Karachi, Pakistan, na kutangaza mpango wa kuimarisha usalama katika maeneo ya kufanyia kazi, ili kuepukana na mkasa kama huo siku zijazo.

Francesco d’Ovidio, ambaye ni Mkurugenzi wa ILO nchini Pakistan, ameuzuru mji wa Karachi siku ya Ijumaa na kukutana na Gavana wa jimbo la Sindh. Ametoa rambi rambi zake kufuatia vifo vya wafanyakazi wengi tu, na kuelezea jinsi ILO itakavyozisaidia familia za waathirika, na idara ya wafanyakazi ya Sindh.

Wakati moto ulipozuka kwenye kiwanda hicho cha nguo, wengi wa wafanyakazi hao walikwama ndani mwa jengo kwa sababu hakukuwa na milango ya kutokea kwa dharura wakati wa moto, na madirisha yalikuwa yamezibwa. ILO imetoa wito kurejeshwe mfumo wa ukaguzi wa hali ya wafanyakazi katika viwanda vyote, na itaisaidia idara ya wafanyakazi ya Sindh kuwa na uwezo wa kufanya ukaguzi kama huo.