Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera za kiserikali bado zahitajika kuchagiza maendeleo kufuatia Mdororo wa kiuchumi:UNCTAD

Sera za kiserikali bado zahitajika kuchagiza maendeleo kufuatia Mdororo wa kiuchumi:UNCTAD

Sera za kiserikali za kubana matumizi ya fedha pamoja na mishahara kupungua, vinasababisha kuendelea kudhoofisha maendeleo katika nchi zilizoendelea bila kupata matokeo yaliyotarajiwa ya kupunguza madeni, kupanua nafasi za ajira na kuongeza matumaini katika masoko ya fedha, imesema ripoti ya Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, ya mwaka 2012.

Ripoti hiyo inayohusu sera za ukuaji bora na ambao unawahusisha wote, imechapishwa leo, na inaangazia hasa kutokuwepo usawa katika riziki na kusema kwamba, kupunguza pengo la kiujira na mali hakutaleta tu manufaa ya kijamii, bali pia kutachangia ukuaji mkubwa wa kiuchumi.

Ikirejelea mwenenendo wa matukio katika uchumi wa kimataifa, ripoti hiyo inaonya kuwa ukuaji wa kicuhumi umepungua katika maeneo yote ya ulimwengu, na hasa kwa sababu ya sera za kubana matumizi ya fedha ambazo zinapunguza uwezo wa watu kununua vitu katika masoko ya nchi zilizoendelea. Ukuaji wa kimataifa ulishuka kutoka asilimia 4.1 mwaka 2010 hadi asilimia 2.7 mwaka 2011, kwa mujibu wa takwimu za ripoti hiyo. Kiwango hiki cha kushuka viwango vya ukuaji kinatarajiwa kufika chini ya asilimia 2.5 mwaka huu, kwa mujibu wa UNCTAD.