Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya simu za mkononi na huduma zake zinawasaidia watu wenye ulemavu kupata fursa mpya:ITU

Teknolojia ya simu za mkononi na huduma zake zinawasaidia watu wenye ulemavu kupata fursa mpya:ITU

Mitazamo ya ubunifu kutoka kwa waundaji wa simu za mkononi hna matumizi yake pamoja na waendeshaji wanasaidia kuwaunganisha takribani watu asilimia 15 duniani na uwezo wa taarifa na teknolojia ya mawasiliano ambao wnaishi na aina Fulani ya ulemavu.

Ripoti mpya iliyotolewa na kwa ushirikiano wa muungano wa teknolojia ya mawasiliano duniani ITU na mshirika wa jumuiya za kijamii zinazojumuisha pande zote katika masuala ya teknolojia ya mawasiliano G3ict, kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa haki za watu wenye ulemavu unaofanyika New York kuanzia leo hadi tarehe 14 mwezi huu , imeonyesha hamasa kubwa ya kuwa na teknolojia itakayotoa fursa ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kuwasiliana, kupata taarifa na kudhibiti mazingira yao.

Ripoti inasema mara nyingi wazee, watu wenye ulemavu na wasijua kusoma wala kuandika huachwa kando na teknolojia ya simu za mkononi,kwa sababu simu hizo hazina nyezo za kuyawezesha makundi haya ya watu kuzitumia, au gharama ni kubwa sana na makundi haya hayawezi kumudu kununua.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mambo hivi sasa yanabadilika kukiwa na ari, hamasa na matumaini ya kuwa na machaguo mbalimbali yanayokuja hivi sasa katika soko la simu za mkononi na teknolojia nyingine zinazoweza kuyashirikisha makundi haya kufurahia maendeleo ya teknolojia.