Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majeshi ya Syria yanawalenga watoto:Zerrougui

Majeshi ya Syria yanawalenga watoto:Zerrougui

Majeshi ya Syria yameongezwa katika orodha ya Umoja wa Mataifa ya pande zinaouwa au kulemaza watoto. Kwa mujibu wa mwakilishi mjaalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto na vita vya silaha Leila Zerrougui amesema kuna ushahidi kwamba majeshi ya Syria wakiwemo wanamgambo wake maarufu wa Shabbiha wamekuwa wakiwalenga watoto.

Bi Zerrougui amesema ofisi yake pia imepoka ripoti ambazo hazijathibitishwa za kuwaingiza watoto jeshini na mauaji ya watoto yanayofanywa na majeshi ya upinzani. Akiwasilisha ripoti yake kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva mwakilishi huyo maalumu amezitaka nchi zote kuharakisha sheria ambazo zinapinga vikali na kufanya kuwa makosa ya jinai kuingiza na kutumia askari watoto vitani na pia matumizi ya nguvu.

(SAUTI YA LEILA ZERROUGUI)