Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaweka mpango sahihi wa kumulika hali ya uhamiaji Jamaica

IOM yaweka mpango sahihi wa kumulika hali ya uhamiaji Jamaica

Mwongozo uliowekwa nchini Jamaica na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM ambao unamulika mwenendo wa uhamaji na uhamiaji umedhibitisha kuwa idadi kubwa ya watu wanaoingia nchini wakijihusisha na usakaji kazi hawakai huko kwa kipindi kirefu.

Ama mwongozo huo umebaini kuwepo kwa ongezeko kubwa la watu wanakwenda nje ya nchi ijapokuwa kiwango hicho siyo kikubwa kikilinganishwa na kile cha miongo kadhaa ya nyuma.

Katika kipindi cha kuanzia miaka ya 1970 hadi miaka 90, kiwango cha Wajamaica waliosafiri kuelekea Marekani kilifikia zaidi ya asilimia 80.33, wakati wale walioelekea nchini Canada kilifikia asilimia 16.96 na nchini Uingereza ilikuwa asilimia 2.71