Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi kipya cha Uganda chatumwa nchini Somalia

Kikosi kipya cha Uganda chatumwa nchini Somalia

Jeshi la Uganda limetuma wanajeshi 2831 kwenda nchini Somalia kupigana na wanamgambo wa al Shabaab. Wanajeshi hao ambao ni kundi la kumi wanaelekea nchini Somalia kuchukua mahala wa kundi la nane ambalo limekuwa likipambana na wanamgambo kwenye taiafa hilo la pembe ya Afrika.

Wanajeshi kutoka kikosi cha AMISON nchini Somalia pia wamepelekwa kwenye bandari ya Elma’an iliyo umbali wa kilomita 40,000 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Mogadishu huku kikosi hicho kikiendelea kudhibiti maeneo zaidi kutoka kwa wanamgambo. Kulingana na AMISOM bandari hiyo imekuwa ikitumiwa na wanamgambo katika kuingiza silaha haramu pamoja na wapiganaji kutoka Ghuba ya Aden.