Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wanaoishi na virusi vya HIV wanasauliwa wakati wa majanga dharura

Watu wanaoishi na virusi vya HIV wanasauliwa wakati wa majanga dharura

Afisa mmoja wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR ambaye anahusika na masuala ya virusi vya HIV amesema kuwa wakati tatizo la ukame lilipoangukia katika eneo la pembe ya Afrika na kuacha eneo hilo kusalia kwenye hitajio la chakula, na wakati machufuko baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya na kusababisha watu zaidi ya 700,000 kwenda uhamishoni, ukweli wa mambo ni kwamba watu walioathiriwa zaidi na matukio hayo ni wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Wakati wa majanga ya dharura, watu wanaweza kupoteza mwelekeo halisi juu ya mfumo wao wa kimaisha, na kujikuta wenye shida na kuandamwa na matatizo kama utapiamlo na wengine wakiandamwa zaidi na matatizo ya magonjwa. Katika hali kama hiyo kuna uwezekano wanawake na watoto wakatumbukia kwenye mambo kama ya kuuza miili yao ili kujikimu na chakula, amesema says Sathya Doraiswamy.

Ametaka kuchukuliwa kwa hatua zenye kuwatupia macho watu wanaishi na virusi vya HIV hasa wakati kunapojitokeza majanga ya dharura. Ameongeza kusema kuwa ili kufikia shabaha ya kukabiliana na maambukizi mapya kuna haja ya kuwafilikia watu ambao tayari wamepata maambukizi hayo.