Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumla ya wakimbizi 100,000 walihama Syria Agosti

Jumla ya wakimbizi 100,000 walihama Syria Agosti

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema kuwa zaidi ya raia 100,000 wa Syria waliikimbia nchi yao mwezi Agosti ukiwa ndio mwezi wenye kiasi kikubwa zaidi ya raia wa Syria waliahama nchi yao tangu kuanza kwa mzozo.

Hadi sasa karibu wasyria 234,000 wamekimbilia mataifa jirani yakiwemo Jordan, Lebanon, Iraq na uturuki.Nchini Syria hali mbaya ya usalama imekuwa kizuizi cha kufikia familia zinazohitaji misaada ya kibinadamu.

Melissa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa shirika hilo kwa ushirikiano na shirika la mwezi mwekundu wamezindua mpango za kufikia familia zilizohama makwao na kuzisaidia kununua chakula na katika kupata mahitaji mengine kuhimu.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)