Mtaalamu wa UM aitaka Ufaransa kuheshimu sheria za kimataifa

30 Agosti 2012

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya haki ameitaka serikali ya Ufaransa kutoziendelea kinyume sheria za kimataifa zinazoangazia kutokuwepo kwa ubaguzi wakati inapotekeleza hatua ya kuyahamisha makazi ya Kiroma na kuwarejesha wahamiaji wake.

Ufaransa imedaiwa kuendesha operesheni ya kuwarejeresha makwao wahamiaji kadhaa ikiwemo wale walioko katika miji ya Lille, Lyon na Paris.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa Raquel Rolnik amelaani kitendo cha kuwahamisha kwa nguvu wahamiaji hao akisisitiza kuwa Ufaransa inapaswa kuziheshimu sheria za kimataifa.

Mtaalamu huyo ameeleza pia kitendo kama hicho kiliwahi kufanywa miaka kadhaa ya nyuma.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud